Pata taarifa kuu
NIGERIA

Kundi la maharamia la Boko Haram lakataa wito wa rais Goodluck Jonathan.

Kundi la maharamia la Boko Haram limekataa wito wa rais Goodluck Jonathan kulitaka kundi hilo kujitokeza hadharani na kuweka wazi madai yao katika meza ya mazungumzo.

Askari wakiimarisha ulinzi baada ya kundi la Boko Haram kufanya shambulio katika mji wa Kano
Askari wakiimarisha ulinzi baada ya kundi la Boko Haram kufanya shambulio katika mji wa Kano Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi hilo la kiislam Abul Qaqa amekataa wito huo wa rais Jonathan na kutishia kufanya mashambulizi mengine zaidi katika mji wa Sokoto endapo wafuasi wa kundi hilo waliokamatwa hawataachiwa huru.

Serikali ya rais Goodluck Jonathan inakosolewa vikali kutokana na kushindwa kulidhibiti kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likitekeleza mashambulio katika taasisi za dini na vituo vya usalama nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.