Pata taarifa kuu
SYRIA

Jumuiya ya nchi za kiarabu yasitisha Operesheni yake nchini Syria.

Jumuiya ya nchi za kiarabu imesema inasitisha operesheni ya waangalizi wake nchi Syria kufuatia kuongezeka kwa machafuko nchini humo.

Mkuu wa operesheni nchini Syria  Amed Mustafa al Dabi
Mkuu wa operesheni nchini Syria Amed Mustafa al Dabi en.rian.ru
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa ujumbe wa waangalizi hao nchini Syria Ahmed Mustafa al Dabi amesema kuwa machafuko yanayoendelea hayasaidii kuzileta pande zote mbili katika meza ya mazungumzo.

Hatua ya kusitishwa kawa operesheni hiyo inakuja siku moja baada ya taarifa ya kiongozi huyo kubainisha kuwa machafuko yameongezeka zaidi juma hili hasa katika miji ya Homs, Hama na Idlib.

Taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo zitatolewa hapo baadaye.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.