Pata taarifa kuu
SYRIA-UMOJA WA MATAIFA

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwenda Umoja wa Mataifa UN kusaka uungwaji mkono juu ya Syria

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inatarajia kuendelea na Shinikizo lake la kusaka uungwaji mkono kutoka kwa Umoja wa Mataifa UN lengo likiwa ni kutaka kusitishwa kwa umwagaji wa damu ambao umekuwa ukishuhudiwa.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Nabil Al Arabi na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Hamad Bin Jassim Al Thani ndiyo watakwenda New York kwa ajili ya kuteti na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaka mbinu za kudhibiti kile kinachoshuhudiwa nchini Syria.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Nabil amesema watakuwa na kikao na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon kwa nyakati tofauti.

Nabil ameweka bayana msimamo wao ungali ni kumtaka Rais Bashar Al Assad akabidhi madaraka kwa msaidizi wake ili mchakato wa mabadiliko uanze nchini Syria na kupata suluhu ya ghasia zilizodumu kwa miezi kumi na moja sasa.

Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu waliagiza kwa kauli moja kutaka Rais Assad akae kando kitu ambacho kilipingwa vikali na Waziri wa Mambo ya Nje Walid Al Mullem.

Katika hatua nyingine taarifa ambazo zimetolewa na wanadiplomasia wa Ufaransa zinasema kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuwa na kikao cha siri cha kujadili machafuko yanayoendelea nchini Syria.

Wanadiplomasia hao wamezungumza kwa sharti la kutotajwa majina wamesema kile ambacho kitajadiliwa ni pamoja na hatua za kuchukuwa baada ya kuonekana juhudi kadhaa kugonga mwamba nchini humo.

Mkutano huo huenda ukafanyika kabla ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu hazijawakilisha pendekezo lake la kuchukuliwa hatua kwa Utawala wa Rais Bashar Al Assad unaotajwa kukosa uhalali wa kiuongozi.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu tano na mia nne wamepoteza maisha nchini Syria tangu kuanza kwa machafuko yaliyodumu kwa miezi kumi na moja sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.