Pata taarifa kuu
UFARANSA

Mgombea Urais Nchini Ufaransa Francois Hollande aanza kampeni zake na kuahidi kuongeza kodi kwa matajiri

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Kisoshalisti nchini Ufaransa Francois Hollande ameahidi kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa matajiri na kuondoa mamilioni ya kodi ambayo uamekuwa yakielezwa kwa wananchi maskini.

AFP PHOTO PATRICK KOVARIK
Matangazo ya kibiashara

Hollande ametoa kauli hiyo wakati akianza rasmi harakati zake za kampeni za kuwania urais wa nchi hiyo ambapo amechukua nafasi hiyo kuanika sera zake ambazo anaamini zitawaondolewa hali ngumu wananchi wa kipato cha chini.

Hollande ambaye anaonekana kupigwa chapuo kumuondoa madarakani Rais wa sasa Nicolas Sarkozy kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Urais ambacho kitafanyika mwezi May mwaka huu ameonekana kuguswa zaidi na suala la uchumi.

Mgombea huyo kipitia Chama Cha Kisoshalisti ameahidi kukabiliana na deni la nchi hiyo kufikia mwaka 2017 kwa kiwango kikubwa zaidi tofauti na ambavyo serikali iliyopo madarakani ilivyofanya.

Ilani ya Uchaguzi ya Hollande ambaye anaongoza kwanye harakati za kuunasa urais wa Ufaransa imejaa mikakati mbalimbali ikiwemo ni pamoja na kutengeneza ajira laki sita za walimu.

Hollande ameweka bayana nia yake ni kutaka kuwa Rais wa kwanza kutoka Chama hicho cha Kisoshalisti katika kipindi cha miaka kumi na saba licha ya upinzani ambao huenda akakutana nao kutoka kwa Rais Sarkozy.

Mkurugenzi wa Kampeni wa Hollande, Pierre Moscovici amesema wamebaini uwepo wa njama za wapinzani wao kutaka kutoa takwimu za uongo na kuwapotosha wapigakura ambao wanania ya dhati kumchagua mgombea wao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.