Pata taarifa kuu
UFARANSA-UTURUKI

Bunge la Seneti la Ufaransa lapitisha muswada wa mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Armenia

Bunge la Senati nchini Ufaransa hatimaye limepitisha muswada wa kutambua Uturuki ilitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Armenia na kuchangia vifo vya watu zaidi ya milioni moja na nusu wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia kati ya mwaka 1915 hadi 1916.

Matangazo ya kibiashara

Kupitishwa kwa muswada huo kumepokelewa kwa mtazamo tofauti na nchi hizo mbili wakati Armenia inasema hatua hiyo ni ya kihistoria na thamani yake inafaa kupewa maandishi wa dhahabu lakini Uturuki imekasirishwa mno na kitendo hicho cha Bunge la Senati.

Masenata katika Bunge hilo wamepiga kura mia moja na ishirini na saba kupitisha muswada huo ambao sasa unawabana wale ambao hawatambui mauaji hayo kama ya kimbari na yoyote atakayekana huenda akafungwa mwaka mmoja au akapigwa faini ya euro 45.

Uturuki imekuwa mbogo na kusema bayana kuwa haikubaliani na uamuzi huo wa Bunge la Seneti la Ufaransa na imesema kuna kila dalili uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo huenda ukatetereka.

Tayari uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo ulishaanza kuingia dosari mwezi uliopita kufuatia Ufaransa kuanzisha mkakati huo wa kutambua Uturuki ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Armenia.

Waziri wa Sheria wa Uturuki Sadullah Ergin ameiambia Televisheni ya Taifa kuwa hatua hiyo inakwenda kinyume cha sheria na kimedhihirisha ukosefu wa heshima kwa nchi hiyo kulikofanywa na Ufaransa.

Waziri Ergin amesema wanalaani vikali hatua hiyo ya Bunge la Seneti nchini Ufaransa kupitia muswada huo wa kutambua nchi yao iliketekeleza mauaji ya kimbari wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia.

Muswada huo unatarajiwa kukabidhiwa kwa Rais Nicolas Sarkozy ili aweze kusaini na hatimaye iweze kuwa sheria ambayo itakuwa inatumika katika nchi hiyo na kuwa kibano kwa wale ambao hawatambui mauaji hayo kama ya kimbari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.