Pata taarifa kuu
SYRIA-MISRI

Syria yakataa Mpango wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wa Rais Assad kukabidhi madaraka kwa Makamu Wake

Serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al Assad imekataa mpango wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kumtaka Kiongozi wa nchi hiyo kukabidhi madaraka kwa Makamu wake ikiwa ni juhudi za kumaliza umwagaji wa damu ambao unaendelea kuchacha.

REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Afisa Mmoja wa Serikali ya Syria amenukuliwa kwenye Televisheni ya Taifa nchini humo akisema pendekezo hilo la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limeketaliwa na serikali yakekwani linaingia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Afisa huyo amesema kitendo cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kutaka Rais Assad kukabidhi madaraka kwa Makamu wake ni sawa kabisa na kushambulia uhuru wa dola hiyo kwenye mambo yake ya ndani.

Hatua ya serikali ya Syria kukataa mpango wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu umekuja siku moja baada ya kufanyika kwa mkutano wa jumuiya hiyo huko Cairo nchini Misri na kupendekeza Makamu wa Rais achukue madaraka katika kipindi cha miezi miwili.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu baada ya kupitisha uamuzi huo wakataka wapate ushirikiano kutoka Umoja wa Mataifa UN kwani wanaamini hiyo ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuwa suluhu ya umwagaji wa damu unaoendelea kwa sasa.

Taarifa ambayo ilitolewa na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Hamad Bin Jassim Al Thani baada ya kukamilika kika cha Mawaziri wa Mambo ya Nje imesema wanataka serikali ya Umoja iwe imeundwa katika kipindi cha mwezi mmoja.

Sheikh Al Thani ameweka bayana kuwa mara tu Rais Assad atakapokabidhi madaraka kwa Makamu wake ndani ya miezi miwili wapinzani watashirikishwa kwenye serikali ya muda ya umoja kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi.

Serikali ya Syria imejibu hilo kwa kusema Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inataka kuharibu zaidi hali ya kisiasa katika taifa hilo na haliwezi kuwalinda wananchi wa nchi hiyo kazi ambayo itaendelea kufanywa na serikali.

Hatua hiyo inakuja baada kukamilika kwa mwezi mmoja wa waangalizi wa Jumuiya ya Nchi zaKiarabu ambao walikuwepo nchini Syria kuangalia hali ilivyo ili kufikishwa ripoti katika jumuiya hiyo na hivyo kupata njia ya kumaliza machafuko.

Takwimu zinaonesha kuwa watu wanaokadiriwa kufikia elfu sita wamepoteza maisha nchini Syria tangua kuanza kwa machafuko yakushinikiza kuondoka madarakani kwa Utawala wa Rais Bashar Al Assad yaliyodumu kwa zaidi ya miezi kumi na moja sasa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.