Pata taarifa kuu
LIBYA-UHOLANZI

Mahakama ya ICC yakana kuwa na makubaliano na Libya kumhukumu Seif Al Islam

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC imekataa uwepo wa makubaliano na nchi ya Libya kuridhia Mtoto wa Kiongozi wa nchi hiyo Marehemu Kanali Muammar Gaddafi, Seif Al Islam ahukumiwe katika mahakama za nchi hiyo.

Ammar El-Darwish/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya ICC imekanusha vikali uwepo wa makubaliano hayo kujibu kile ambacho kimeelezwa na Waziri wa Sheria wa Libya Ali H'mida Ashur ambaye amesema Seif Al Islam atahukumuwa kwenye Mahakama za ndani.

Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita Fadi El Abdallah amesema hakuna makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa baina yao na nchi ya Libya juu ya kesi inayomkabili Al Islam.

Waziri wa Sheria wa Libya Ashur alinukuliwa akisema kuwa mashtaka ya Al Islam yatasikilizwa nchini Libya kwani mahakama za nchi hizo zinauwezo wa kutosha na kisha watawasilisha faili huko ICC.

Ashur alienda mbali zaidi na kusema kuwa wamekubaliana na Mahakama ya ICC juu ya mpango huo wa kusikiliza kesi ya Al Islam ambaye alikamatwa mwezi Novemba mwaka jana wakati wa harakati za kuuangusha Utawala wa baba yake.

Kauli ya serikali ya Libya kupitia Waziri wake mwenye dhamana na mambo ya sheria imekuja wakati ambapo Mahakama ya ICC ilikuwa inatarajia kuambiwa ni lini watakabidhiwa mtuhumiwa huyo wa makosa ya uhalifu wa kivita.

Mahakama ya ICC ilishatoa waranti ya kukamatwa kwa Al Islam lakini baadaye ikakiri haijui kama kukamatwa kwake kunauhusiano na waranti ambayo waliotoa wakati huu ambapo mtoto huyo wa Kanali Gaddafi akishikiliwa kwenye kambi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.