Pata taarifa kuu
MYANMAR

Human Right Watch yasema jeshi la Myanmar liliwaua raia.

Shirika la kutetea haki za binadamu duniani Human Right Watch limesema kuwa jeshi la serikali ya Myanmar liliwaua na kuwanyanyasa raia pamoja na kuwabaka katika mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini humo licha ya mabadiliko yaliyopo hivi sasa.

Ramani ya nchi ya Myanmar zamani Burma
Ramani ya nchi ya Myanmar zamani Burma travel.nationalgeographic.com
Matangazo ya kibiashara

Vita hivyo vilivyosababisha umwagaji damu vilianza mapema mwezi June katika jimbo la Kachin eneo la kaskazini na kuharibu mchakato wa utawala mpya ambao umewashangaza waangalizi kutokana na mfululizo wa mabadiliko katika nchi hiyo ambayo pia ilijulikana kama Burma.
Katika ripoti yake dhidi ya nchi hiyo shirika hilo limesema kuwa jeshi la Myanmar limeendelea kukiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu kwa kutumia mabomu dhidi ya raia, kujichukulia sheria mikononi, utumikishwaji ,unyanyasaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

Aidha ripoti hiyo imebainisha kuwa ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana duniani bado ni tatizo kubwa wakati jeshi linaendelea kuwaajiri watoto kuwa wanajeshi.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo zaidi ya raia elfu hamsini wameyakimbia makazi yao huko Kachin kutokana na mapigano na kusababisha kusitishwa kawa mapigano hayo yaliyodumu kwa miaka 17 wakati raia wapatao laki tano waliyakimbia makazi yao kutokana na mapigano ya mwaka uliopita katika maeneo ya mpaka mashariki mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.