Pata taarifa kuu
SYRIA

Waangalizi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu wamaliza muda wao nchini Syria.

Syria inasema inaweza kukubali waangalizi kutoka muugano wa nchi za kiarabu ambao wamekuwa wakishutumiwa kushindwa kumaliza machafuko nchini humo kuendelea kuchunguza machafuko yanayoendelea kati ya waandamanaji na majeshi ya serikali.

Waangalizi wa jumuiya ya kiarabu nchini Syria
Waangalizi wa jumuiya ya kiarabu nchini Syria euronews.net
Matangazo ya kibiashara

Muda uliokuwa umewekwa na muungano huo umemalizika na tayari waangalizi hao wamewasilisha ripoti yao kwa viongozi wa umoja huo mjini Cairo Misri.

Mawaziri wa nchi za kigeni wa muungano wa nchi za kiarabu wanatarajiwa kujadili ripoti ya waangalizi hao katika kikao cha siku ya Jumapili kuona ikiwa watawaongezea muda zaidi waangalizi hao kuwa nchini Syria.

Machafuko hayo ambayo yalianza mwezi Machi mwaka uliopita yamesababisha zaidi ya watu elfu tano kuuawa kwa mujibu wa umoja wa mataifa.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy leo Ijumaa amesema Ufaransa haitasalia kimya kuona mauji ya waandamanaji wanaotaka demokrasia nchini Syria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.