Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFGHANISTAN

Ufaransa yasitisha mafunzo kwa askari wa Afghanistani.

Ufaransa imeamua kuahirisha mpango wa mafunzo kwa askari wa afghanstan baada ya kutokea mauaji ya askari wake wanne huko mashariki mwa Afghanstan.

French soldiers in Afghanistan
French soldiers in Afghanistan presstv.ir
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umekuja sambamba na kauli ya Raisi wa Ufaransa Nicolus Sarkozy ambaye amesema kuwa kitendo cha askari wa Afghan kushambulia askari wa Ufaransa hakikubaliki hata kidogo.

Chanzo kimoja cha usalama kilisema Mpaka sasa askari wa Ufaransa wameimarisha ulinzi kuzunguka kambi yao ya Kapisa na kuzuia askari yeyote wa Afghan kukaribia ambapo tayari mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na jeshi la msaada wa usalama kimataifa,ISAF.

Idadi ya majeruhi 16 imepatika katika shambulio la ijumaa katika wilaya ya Tagab,kaskazini mwa mji mkuu wa Kabul kilisema chanzo kwa masharti ya kutojulikana.

Mashambulizi yalitokea ndani ya kambi wakati wa kikao cha mafunzo yanayoendeshwa na majeshi ya Ufaransa na taarifa zinasema kuwa idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.

Matukio ya mauaji yalianza kuchomoza mapema mwezi uliopita baada ya askari 2 wa Ufaransa kushambuliwa na mtu aliyevalia sare za jeshi la Afghanstan katika eneo la kapisa ambalo ni kambi ya askari wa Ufaransa.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.