Pata taarifa kuu
UGANDA

Jeshi la polisi nchini Uganda lamkamata tena kiongozi wa upinzani Kizza Besigye

Jeshi la Polisi nchini Uganda linaendelea kumshikilia kiongozi mkuu wa upinzani daktari Kizza Besigye aliyekamatwa katika jiji la Kampala wakati akijaribu kuanzisha upya kampeni yake ya kutaka serikali idhibiti kupanda kwa gharama za maisha.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Judith Nabakooba amekiri kukamatwa kwa daktari Besigye na viongozi wengine wanne wa upinzani ambao walikuwa wanataka kufanya maandamano yasiyo na kibali.

Punde baada ya kukamatwa daktari Besigye akaendelea kuishutumu serikali kutokana na kukandamiza haki zao na kusema kuwa wataendelea kupaza sauti zao ili kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.