Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Mahakama nchini Pakistani kumchunguza waziri mkuu Gilani.

Waziri Mkuu wa Pakistan Yousef Raza Gilani amefika mahakamani kujieleza ni kwanini alipuuza uamuzi wa mahakama wa kutaka serikali kuanza uchunguzi dhidi ya kashfa za ufisadi zinazomkabili rais Asif Ali Zardari.

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari.
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari. elegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Gilani amewaambia majaji wa mahakama ya rufaa kuwa nia yake si kuidharau mahakama bali hajaanza mchakato wa kumchunguza rais Zardari kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo ambayo inatoa msamaha kwa rais.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 1 mwezi ujao,na ikiwa waziri huyo mkuu atapatikana na hatia atapigwa marufuku ya kuhodhi ofisi ya umma.

Rais Zardari na marehemu mkewe Benazir Bhutto walipatikana na kosa la kuhusika na biashara haramu ya fedha mwaka 2003 na serikali ya Uswizi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.