Pata taarifa kuu
NIGERIA

Serikali ya Nigeria yaridhia mazungumzo na vyama vya wafanyakazi

Rais wa Nigeria Gudluck Jonathan amejipanga kukutana na umoja wa vyama vya wafanyakazi jumamosi kwa ajili ya kurejesha utulivu baada ya kuwepo kwa maandamano na mgomo nchini humo kupinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta iliyosababisha kupanda kwa gharama za mafuta nchini humo.

Wananchi nchini Nigeria wakiandamana kupinga sera ya serikali ya raisi Goodluck Jonathan kupanda gharama za mafuta
Wananchi nchini Nigeria wakiandamana kupinga sera ya serikali ya raisi Goodluck Jonathan kupanda gharama za mafuta REUTERS/Akintunde Akinleye
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa wafanyikazi nchini humo unasema mgomo utaendelea hadi pale serikali yake itakaposikia kilio chao.

Kiongozi wa chama hicho Babatunde Ogun amesema kuwa ikiwa maeneo ya uzalishaji wa mafuta na gesi yatafungwa itachukua miezi sita kuanza tena uzalishaji.

Wananchi wa Nigeria wamekuwa katika maandamano wakipinga sera ya ruzuku ya mafuta iliyosababisha kupanda kwa gharama za nishati hiyo,sera iliyotangazwa na serikali ya raisi Goodluck Jonathan.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.