Pata taarifa kuu
ALGERIA

Watu kumi wajeruhiwa katika vurumai Algeria

Polisi nchini Algeria wamewasambaratisha kwa kuwamwagia gesi ya machozi waandamanaji waliokuwa na hasira juu ya namna taifa hilo linavyokabili hali ya ukosefu wa ajira na makazi kusini mwa nchi hiyo vurumai zilizosababisha watu kumi kujeruhiwa katika eneo la Laghouat.

Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika
Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika AFP/Fayez Nureldine
Matangazo ya kibiashara

Shirika linalotetea haki za binaadam la Algerian League for defence of Human Rights ,ALDHR limesema Vikosi vya usalama vimewakamata waandamanaji ambao idadi yake haijajulikana.

Rais wa taifa hilo Abdelaziz Bouteflika aliahidi kuwa zaidi ya watu milioni moja watapatiwa nyumba za gharama nafuu katika mpango wa miaka mitano ya mradi wa makazi utakaoisha mwaka 2014, lakini mchakato huo umeelezwa kwenda sambamba na vitendo vya rushwa na kasi ndogo ya ujenzi wa nyumba hizo.

hali ya ukosefu wa ajira nchini Algeria miongoni mwa vijana ilifikia asilimia hamsini miaka kumi iliyopita, na hivi kwa mujibu wa takwimu za shirika la fedha duniani, IMF sasa takribani asilimia ishirini ya raia hawana ajira nchini humo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.