Pata taarifa kuu
NIGERIA

Sita wafariki katika maandamano ya kupinga sera ya serikali Nigeria

Watu sita wameuawa nchini Nigeria na wengine kujeruhiwa baada ya maelfu ya waandamanaji kujitokeza katika miji mbalimbali kupinga hatua ya serikali ya rais Goodluck Jonathan kuondoa ruzuku ya mafuta.

Raisi wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Raisi wa Nigeria, Goodluck Jonathan REUTERS/ Daniel Munoz
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Nigeria walindamana katika mitaa mbalimbali ya mjini Lagos kudhihirisha hasira yao dhidi ya sera ya serikali ya Nigeria iliyosababisha bei ya mafuta nchini humo kupanda mara mbili zaidi.

Wanasheria, madaktari ,wanafunzi , walimu , wafanya biashara ndogondogo na wanawake wachuuzi waliandamana kuonesha kutokubaliana na serikali ya Goodluck Jonathan.

Polsi walikabiliana na waandamanaji hao ambao wanasema wataendelea kuandamana hadi pale matakwa yao yatakaposikika.

Nigeria,ni nchi inayozalisha mafuta zaidi barani Afrika, inaelezwa kuwa na miundo mbinu mibovu ya barabara na umeme huku raia wake wengi wakiishi kwa kiwango cha chini ya dola mbili kwa siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.