Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Raia 35 wauawa katika shambulio nchini Pakistan

Watu 35 wamepoteza maisha na wengine 60 wamejeruhiwa nchini Pakistan kufuatia kutokea kwa shambulio la bomu liliotegwa katika gari, tukio ambalo ni baya zaidi kutoea katika kipindi cha miezi kadhaa ya mashambulizi ya kundi la Taliban katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.

Wasamaria wema wakijaribu kuwaokoa majeruhi wa shambulio nchini Pakistan
Wasamaria wema wakijaribu kuwaokoa majeruhi wa shambulio nchini Pakistan AFP/Photo
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea katika eneo la soko mjini Jamrud,mji ambao ulitumika kama njia kuu ya kusafirishia vikosi vya wanajeshi wa majeshi ya nchi za Magharibi NATO waliokuwa wakiendesha operesheni yao nchini Afghanistan.

Maofisa nchini humo wamesema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na watoto wawili wenye umri wa mika tisa na kumi pamoja na askari wa jadi wapatao watatu.

Hata hivyo hakuna taarifa zilizopatikana kuhusu wahusika wa shambulio hilo ingawa wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa mgogoro wa kikabila huenda ikawa chanzo cha shambulio hilo kwani wengi wa waathirika ni watu wa kabila la Zaka Khel ambao wanampinga kiongozi wa jadi Mangal Bagh.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.