Pata taarifa kuu
ALGERIA

Waziri mkuu wa Algeria, Ahmed Ouyahia akataa kujiuzulu kwa shinikizo la upinzani

Waziri mkuu wa Algeria,Ahmed Ouyahia amesema kuwa hatajiuzulu kwa shinikizo la vyama vya upinzani vinavyodai kuundwa kwa serikali mpya itakayoliongoza taifa hilo kwenye uchaguzi mwezi Mei mwaka huu.

Waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia
Waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia
Matangazo ya kibiashara

Ouyahia amesema uamuzi wa kuvunja serikali uko mikononi mwa aliyeichagua.

Vyama kadhaa vya upinzani vimetaka kuundwa kwa serikali ambayo haitaegemea upande wowote na kusaidia katika kuuwezesha uchaguzi mkuu kuwa wenye kuaminika na wa wazi.

Rais wa Algeria,Abdelaziz Bouteflika aliahidi kufanya mabadiliko kadhaa ya kisiasa na katiba kabla ya mwisho wa mwezi huu ili kukuza Demokrasia ya taifa hilo wanapoelekea kwenye uchaguzi.

Bouteflika amewaalika waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa watakaoangalia mwenendo wa kura za ubunge ambazo ameahidi kuwa zitakuwa za wazi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.