Pata taarifa kuu
BERLIN

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wajipanga kupambana na madeni

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamekubaliana kupambana na kupata fungu zaidi la fedha kuzisaidia nchi ambazo zinakabiliwa na madeni kwenye Ukanda wa Ulaya.

Raisi wa Ufaransa,Nicolaus Sarkozy
Raisi wa Ufaransa,Nicolaus Sarkozy REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya viranja hao wa Ukanda wa Ulaya imekuja wakati walipokutana huklo Berlin wakiwa na lengo la kushughulikia mgogoro wa uchumi ambao unashuhudiwa kwenye mataifa kadhaa Barani Ulaya kwa sasa.

Rais Sarkozy amesema umefika wakati kwa mataifa hayo kuhakikisha yanasimama kidete kuzisaidia nchi nyingine ambazo zinapita katika wakati mgumu kutokana na kukabiliwa na madeni.

Viongozi hao wamekubaliana kuhakikisha wanalitupia macho suala la kumaliza tatizo la ajira ambaloi limeanza kuwa sugu katika Bara la Ulaya na hata kuzua hofu ya kuanguka kwa uchumi wa Bara hilo.

Kansela Merkel amesema hawatorudi nyuma kwenye mpango wao wa kuzisaidia nchi zenye mzigo wa madeni licha ya uwepo wa upinzani unaotoka kwa mataifa mengine yenye nguvu kwenye Umoja wa Ulaya EU.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.