Pata taarifa kuu
NIGERIA

Nigeria ya upokea mwaka mpya kwa tangazo la hali ya hatari.

Raia nchini Nigeria wameupokea mwaka mpya wa 2012 wakiwa katika hali ya wasiwasi baada ya kutangazwa kwa hali ya hatari katika maeneo yaliyoshambuliwa na kundi la kiislam la Boko Haram, kwa lengo la kumaliza machafuko yanayokua kwa kasi na kuitikisa nchi hiyo.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Tamko la hali ya hatari lililotangazwa na rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan linavipa vyombo vya usalama mamlaka zaidi kuwasaka na kuwakamata,kufunga mipaka ya maeneo yaliyoshambuliwa zaidi na kuongeza nguvu za kijeshi katika kukabiliana na ugaidi.

Tamko hilo limekuja kufuatia mashambulio kadhaa yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislam la Boko Haram katika makanisa ya kikatoliki siku ya sikukuu ya Noeli ambapo watu 49 waliuwawa.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.