Pata taarifa kuu
Afghanistani-Taliban

Rais wa Afghanistani aridhia mazungumzo na wanamgambo wa Taliban

Rais wa Afghanistani Harmid Karzai amesema kuwa anakaribisha mazungumzo kati ya serikali yake na viongozi wa kundi la wanamgambo wa Taliban katika kujaribu kusaka suluhu ya kudumu nchini humo, mazungumzo ambayo yanatarajiwa kufanywa nchini Qatar.

Rais wa Afghanistani Hamid Karzaï, Desemba 6, 2011.
Rais wa Afghanistani Hamid Karzaï, Desemba 6, 2011. Reuters/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Licha ya rais Karzai kutangaza wazi msimamo wa serikali yake wakutaka kufanya mazungumzo na kundi la taliban, viongozi wa kundi hilo wenyewe bado hawajatoa taarifa rasmi endapo watashiriki katika mazungumzo hayo.

Mbali na kukubali kufanya mazungumzo na kundi hilo, rais Karzai pia kwa mara ya kwanza ameunga mkono mapendekezo ya majeshi ya Marekani na Ujerumani ya kujenga kambi kubwa ya kijeshi katika eneo la ghuba ya Qatar uamuzi ambao awali aliupinga kwa madai ya serikali yake kutoshirikishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.