Pata taarifa kuu
Nigeria

Kiongozi wa juu wa kiislam nchini Nigeria awataka viongozi kuwa wavumilivu

Kiongozi wa juu wa dini ya Kiislamu nchini Nigeria Sokoto Muhammada Saad Abubakar ametoa wito kwa wananchi wa Nigeria na viongozi wa makanisa nchini humo kuwa wavumilivu wakati huu ambapo kundi la Boko Haram linaendeleza mashambulizi.

Kiongozi mkuu wa kiislam nchini Nigeria Muhammada Saad Abubakar pamoja na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Kiongozi mkuu wa kiislam nchini Nigeria Muhammada Saad Abubakar pamoja na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya mkutano wake na rais Goodluck Jonathan, Abubakar amewaambia waandishi wa habari kuwa hakuna uhasama wowote uliopo kati ya waumini wa dini ya kiislamu na wakristo kutokana na mashambulizi yanayofanywa na kundi la Boko Haram.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa mashambulizi yanayofanywa na kundi la Boko haram yanalenga kuharibu amani ya nchi hiyo na kuwataka wananchi kuungana kuisaidia serikali kuwafichua mahali walipo wafuasi wa kundi hilo.

Upannde wake rais Goodluck Jonathan mara baada ya mkutano na kiongozi huyo hajazungumza lolote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.