Pata taarifa kuu
IRAN

Wauzaji wa dawa za kulevya wanyongwa nchini Iran.

Watu watano wamenyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha na kuuza dawa za kulevya katika gereza moja kaskazini mwa mji wa Shahrud.

Takwimu za Amnesty International  zaitaja Iran kushika nafasi ya pili katika adhabu ya kunyongwa mwaka 2010
Takwimu za Amnesty International zaitaja Iran kushika nafasi ya pili katika adhabu ya kunyongwa mwaka 2010 ©Amnesty International
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka shirika la habari nchini humo zimeeleza kuwa watu hao raia wa Iran ni wakazi wa miji mbalimbali ingawa taarifa zaidi kuhusu umri wao hazikuweza kutolewa.

Kwa mujibu wa takwimu za vyombo vya habari nchini humo, adhabu hii ya kunyongwa inafikisha idadi ya watu 277 walionyongwa nchini humo kwa mwaka huu pekee.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa watu 388 waliuwawa nchini humo mwaka 2010.

Kwa upande wa shirika la Amnest International limetaja nchi ya Iran kuwa ya pili kutekeleza adhabu ya kunyonga hadi kifo katika mwaka uliopita huku nchi ya China ikishika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo Iran imesema kuwa adhabu hiyo ni muhimu kwa ajili ya kulinda sheria na maagizo na kwamba hutumika baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.