Pata taarifa kuu
SYRIA

Ufaransa wataka waangalizi wa amani kutua mjini Homs.

Ufaransa imewataka waangalizi wa amani wa jumuiya ya nchi za kiarabu kwenda haraka katika mji wa Homs nchini Syria,kufuatia wanajeshi wa serikali kuendelea kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Maelfu ya waandamanaji katika mji wa Homs nchini Syria.
Maelfu ya waandamanaji katika mji wa Homs nchini Syria. REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa imesema kuwa mamlaka mjini Damascus kwa kushirikia na jumuiya ya nchi za kiarabu hazina budi kuruhusu waangalizi hao kufika katika mji wa Homs ambako umwagaji damu umekithiri.

Kundi la kwanza la waangalizi hamsini wanatarajiwa kuwasili nchi Syria hii leo kutekeleza mpango wao wenyelengo la kukomesha machafuko yanayosababishwa na utawala wa rais Bashar Al Assad ingawa milio ya risasi imeendelea kusikika katika mji wa Homs.

Makundi ya wapinzani yamesema kuwa takribani watu 13 wameuwawa hii leo katika mji wa Homs pekee huku maofisa wa shirika la msaada wa kibinadamu la umoja wa mataifa wakisema kuwa zaidi ya watu elfu tano wameuwawa nchini humo katika kipindi cha miezi tisa ya mapigano.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.