Pata taarifa kuu
SUDANI

Serikali ya Sudani imetangaza kumuua kiongozi mkuu wa kundi la waasi.

Serikali ya Sudan imetangaza kufanikiwa kumuua kiongozi mkuu wa kundi la waasi wa Justice and Equality Movement, Khalil Ibrahim aliyekuwa akiendesha mapambano dhidi ya serikali mashariki mwa jimbo la Darfur.

Kiongozi wa kundi la waasi nchini Sudan Khalil Ibrahim
Kiongozi wa kundi la waasi nchini Sudan Khalil Ibrahim AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa habari nchini humo Abdulah Ali Massar amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vilifanikiwa kumuua Ibrahim pamoja na wapiganaji wake zaidi ya 30 katika mji wa Wad Banda ulioko kaskazini mwa mji wa Kordofan ambako wapiganaji wake walikuwa wakisonga mbele kuelekea mji mkuu Khartoom.

Kuuwawa kwa Ibrahim ambaye amepigana vita kwa muda mrefu na serikali ya nchi hiyo kumekuja wakati ambapo ni juzi tu alitangaza kuwa wapiganaji wake wameanza kusonga mbele kuuteka mji mkuu Khartoom na kisha kuipindua serikali.

Khalil Ibrahi anadaiwa kushiriki vita nchini Libya kwa kuusaidia utawala wa marehemu kanali Gadafi lakini alirejea nchini humo hivi karibuni na kutangaza vita dhidi ya serikali akiwa ni kiongozi pekee wa kudi la waasi aliyekataa kutekeleza maazimio ya Doha nchini Qatar ya kusaka amani kwenye jimbo la Darfur.

Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.