Pata taarifa kuu
SYRIA

Vurugu zaidi zaripotiwa nchini Syria wakati waangalizi sab toka Umoja wa nchi za Kiarabu wakiwa wamewasili

Vurugu zimeripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini Syria wakati ambapo ujumbe wa watu saba toka Umoja wa nchi za Kiarabu ukiwa umewasili nchini humo kwaajili ya maandalizi ya kuanza uchunguzi wao.

Baadhi ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya rais Asad nchini Syria
Baadhi ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya rais Asad nchini Syria REUTERS/Omar Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati nchini humo wameripoti kuwa katika miji ya Homs na Hama watu kadhaa wamejeruhiwa na baadhi yao kuuawa na vikosi vya Serikali ambavyo viko kwenye miji hiyo kuwasaka wanajeshi walioasi.

Vurugu hizo zinatokeo wakati ambapo ujumbe wa watu saba toka Umoja wa nchi za Kiarabu umewasili hapo jana nchini humo kwaajili ya maandalizi ya awali ya kuanza kwa ucnunguzi rasmi kama walivyokubalina na Serikali ya Syria.

Ujumbe mwingine wa watu kati ya 40 na 50 wanatarajiwa kuwasili nchini humo siku ya jumamosi kuungana na wajumbe wengine saba ambao tayari wamefika nchini humo kwaajili ya kwenda kwenye maeneo ambayo kunatuhumiwa kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hofu ya kiusalama nchini humo imeendelea kutanda wakati huu ambapo wanajeshi wengi wameendelea kuasi jeshi huku wakimiliki silaha nzito ambazo zinahofiwa huenda zikatumia vibaya na kuzidi kuchochea machafuko zaidi.

Rais Asad ameendelea kusisitiza kuwa hana hatia kutokana na vifo ambavyo vimetokea nchini humo na kuendelea kuwashutumu wanaojiita wanaharakati wa mapinduzi kwa kuchochea vurugu nchini humo.

Siku ya jumatano kuliripotiwa watu mia mbili na hamsini kuuawa katika miji ya Homs na Hama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.