Pata taarifa kuu
SYRIA

Ujumbe wa watu 7 ambao ni waangalizi toka Umoja wa nchi za Kiarabu wamewasili nchini Syria

Ujumbe wa waangalizi saba toka Umoja wa nchi za Kiarabu umewasili nchini Syria tayari kuanza kazi ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za kuwepo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na jeshi la nchi hiyo pamoja na wananchi wanaoipinga serikali.

Syrian refugees carry banners and Syrian flags as they shout slogans during a protest in front of the Red Cross offices in Tripoli, northern Lebanon November 25, 2011.
Syrian refugees carry banners and Syrian flags as they shout slogans during a protest in front of the Red Cross offices in Tripoli, northern Lebanon November 25, 2011. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi hao wanawasili nchini humo huku ikiwa imepita siku moja tu toka wanaharakati nchini Syria waripoti mauaji ya raia mia mbili na hamsini waliouawa kwa kushambuliwa na vikosi vya serikali katika miji mbalimbali.

Kuwasili kwa waangalizi hao kumekuja kufuatia siku ya Jumatatu viongozi wa Serikali ya Syria wakiongozwa na naibu waziri wa mambo ya nje watie saini makubaliano ya kuruhusu waangalizi toka Umoja huo kwenda nchini Syria.

Awali mawaziri toka Umoja huo walitishia kuifuta uanachama nchi ya Syria baada ya kukataa waangalizi wa kimataifa lakini baadae ililegeza msimamo wake na kukubali kutoa mwezi mmoja kwa waangalizi wa Umoja huo kufanya kazi waliyoagizwa.

Wakiwa nchini humo waangalizi hao watatembelea maeneo ambayo yaliripotiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuwahoji wananchi ambao wamepoteza ndugu zao toka machafuko hayo yalipoanza lakini pia watawahoji maofisa wa polisi ambao wanahusika na kutuliza ghasia nchini humo.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Syria Waleed Muallem alinukuliwa hapo juzi wakati akitangaza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu akisema kwamba nchi yake imekubali kuruhusu waangalizi hao sio kwakuogopa hatua za kijeshi ambazo zingechukuliwa na Umoja wa mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.