Pata taarifa kuu
IVORY COAST

Rais Alassane Ouattara afurahia ushindi baada ya uchaguzi kususiwa na wapinzani.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara pamoja na wafuasi wake wamefurahia ushindi waliopata katika uchaguzi uliofanyika siku ya jumapili huku uchaguzi huo ukisusiwa na wafuasi wa mpinzani wake mkuu Laurent Gbagbo.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara. REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Mara baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo Bagbo ambaye ni kiongozi wa chama cha FPI alisema kuwa Ouattara alikuwa mkuu wa utawala haramu na amekuwa madarakani kutokana na mabavu.

Kwa sasa Gbagbo anasubiri kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini Hague Uholanzi, kwa tuhuma za makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu baada ya kukamatwa majeshi ya Rais Ouattara kwa msaada wa nchi ya Ufaransa na majeshi ya umoja wa mataifa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.