Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UINGEREZA

Kansela wa Ujerumani Merkel asisitiza Uingereza ni muhimu katika kutatua matatizo ya Umoja wa Ulaya EU

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameliambia Bunge la Nchi yake Bundestag licha ya kwamba Uingereza imekataa kusaini makubaliano ya Umoja wa Ulaya EU mwishoni mwa juma lililopita bado nchi hiyo ni muhimu katika Ukanda huo.

Reuters/Tobias Schwarz
Matangazo ya kibiashara

Kansela Merkel amewahutubia wabunge wa nchi yake ikiwa ni baada ya nchi hiyo kwa kushirikiana na Ufaransa kuwashawishi nchini wanachama wengine kuridhia mkataba mpya wa kusaidia suala la madeni licha ya Uingereza kukataa.

Merkel ameliambia Bunge la Bundestag kuwa licha ya Uingereza kuonesha dhahiri kutokuwa tayari kusaini mkataba huo ulioidhinishwa na mataifa wanachama ishirini na sita lakini nchi hiyo inahitajika sana kwenye kushughulikia matatizo ya Ulaya.

Kansela Merkel amekwenda mbali na kusema mustakabali wa sarafu ya euro kwa wanachama wake kumi na saba haiwezi kupatikana iwapo nchi ya Uingereza haitoshirikishwa kwenye mchakato huo.

Merkel amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kukataa kusaini mkataba huo lakini hiyo si sababu ya kuiweka kando nchi yake.

Kiongozi huyo wa serikali ya Ujerumani alikuwa anaongea kwa mara ya kwanza kutetea mpango wa nchi yake kuwa mstariwa mbele katika kuhakikisha suluhu ya madeni na hatima ya sarafu ya euro zinapatikana.

Katika hatua nyingi Merkel amesema ni wazi kabisa suluhu ya madeni ikipatikana katika eneo la Ukanda wa Ulaya itasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya haraka na kuziokoa nchi nyingine kama Ugiriki na Italia.

Merkel amesema ifikapo mwaka elfu mbili na kumi na mbili wanataka suala hili liwe limeshapatiwa ufumbuzi na kuondoa tishio la kuzorota kwa uchumi wa dunia.

Ujerumani na Ufaransa zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mgogoro wa madeni unapatiwa suluhu sambamba na hatima ya sarafu ya euro kwa nchi wanachama ambazo zinatumia.

Umoja wa Ulaya EU kwa sasa una jumla ya wanachama ishirini na saba lakini nchi ya Uingereza pekee ndiyo imeonesha ukaidi wa kukubaliana na mkataba mpya wa kufanya mabadiliko kwenye Umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.