Pata taarifa kuu
IRAQ-SYRIA

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zebari asema si rahisi kuiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi.

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zebari amesema kuwa si rahisi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Syria kutokana na uhusiano wa kibiashara uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zebari
Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zebari AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Najaf, Zebari amesema kuwa nchi yake inaona kuwa jambo hilo ni gumu kutekelezeka kauli ambayo haijulikani kama inamaanisha kuwa nchi hiyo haiungi mkono uamuzi wa jumuiya ya nchi za kiarabu kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Syria.

Awali jumuiya ya nchi za kiarabu imetangaza rasmi nia yake ya kuiwekea vikwazo nchi ya Syria baada ya utawala wa rais Bashar Al Assad kushindwa kutekeleza mapendekezo ya jmuiya hiyo ya kutaka waangalizi kuingia nchini humo.

Rais wa nchi hiyo Bashar Al Assad alipinga vikali hatua ya jumuiya hiyo kutaka kuingia nchini mwake.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa watu zaidi ya elfu tatu na miatano wamepoteza maisha nchini humo tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.