Pata taarifa kuu
GAMBIA

Rais Yahya Jammeh afanikiwa kutetea kiti chake cha urais kwa awamu ya nne.

Tume ya uchaguzi nchini Gambia imemtangaza rasmi Yahya Jammeh kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kupata kura zaidi ya asilimia sabini huku mpinzani wake mkuu Ousainou Darboe akipata asilimia 17 ya kura zilizopigwa.

Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Rais wa Gambia Yahya Jammeh IISD/Earth Negotiations Bulletin/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo bwana Ousainou Darboe ametangaza kutokukubali matokeo hayo na kuwataka wananchi kumuunga mkono kwa madai kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki na ulitawaliwa na vitisho dhidi ya wapinzani na wapiga kura.

Rais Yahya ambaye anashutumiwa kwa kuongoza kwa mabavu,aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mnamo mwaka 1994 na akashinda uchaguzi mara tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.