Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-YEMEN

Rais wa Yemen atia saini makubaliano ya kukabidhi madaraka kwa makamu wake

Rais wa Yemeni Ali Abdullah Saleh hatimaye amekubali kusaini makubaliano ya kuondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 33 na sasa atakabidhi ofisi kwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Abdrabuh Mansur Hadi.

Rais wa Yemen akifurahia jambo kabla ya kutia saini makubaliano ya kukabidhi madaraka
Rais wa Yemen akifurahia jambo kabla ya kutia saini makubaliano ya kukabidhi madaraka Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Saleh amefikia uamuzi wa kusaini makubaliano hayo baada ya uwepo wa ghasia katika nchi hiyo zilizodumu kwa miezi kadhaa kutokana na wapinzani kutaka mabadiliko na sasa makamu wa rais atakuwa na siku tisini kuitisha uchaguzi.

Hatua ya ya kujiuzulu imepongezwa na Marekani ambao inataka kuandikwa kwa historia mpya huku wachambuzi wa siasa wakiona huu ni ushindi kwa umma.

Hata hivyo licha ya kusaini makubaliano hayo bado waandamanaji katika mji wa Sanaa wamekataa mapendekezo ya Umoja wa nchi za kiarabu katika ghuba wakisema kuwa makubaliano hayo ni batili kwakuwa yatawaacha watu walioua ndugu zao bila kuchukuliwa hatua.

Wanaharakati na waandamanaji wengine wamenukuliwa wakisema kuwa hawatakubali makubaliano ambayo rais Saleh ametia saini na kwamba wanataka kuona kiongozi huyo akishtakiwa kutokana na makosa ambayo ameyatenda wakati akiwa kiongozi.

Rais Saleh anatarajiwa kung'atuka madarakani mapema mara baada ya kuitishwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo ambapo itashuhudiwa kiongozi huyo pamoja na familia yake kutochukuliwa hatua zozote kwa mujibu wa makubaliano ambayo ametia saini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.