Pata taarifa kuu
UTURUKI

Waokoaji huko Uturuki wamkuta hai mvulana wa miaka 12 baada ya saa 108

Waokoaji wanaofanya zoezi la kusaka miili ya watu na hata wale ambao wameendelea kusalia hai chini ya vifusi nchini Uturuki baada ya Taifa hilo kupigwa na tetemeko la ardhi wamefanikiwa kumuokoa kijana mwenye umri wa miaka kumi na miwili baada ya kunasa kwa saa mia moja na nane.

Matangazo ya kibiashara

Mvulana huyo ametambulika kwa jina la Ferhat Tokay amenasuliwa kutoka katika lundo la vifusi ambavyo vimechangiwa na kuanguka kwa majengo mbalimbali nchini humo baada ya kupingwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa saba nukta mbili katika vipimo vya matetemeko.

Ferhat ameokolewa saa kadhaa baada ya kikosi hicho cha waokoaji kufanikiwa kumnasua Imdat Padak mwenye umri wa miaka kumi na minane ambaye naye alikuwa amefunikwa na vifusi katika Mji wa Ercis.

Watoto hawa wameokolewa wakati huu ambapo Mamlaka Nchini Uturuki zikitangaza takwimu mpya za vifo ambayo imefikia watu mia tano na sabini na watatu huku wengine elfu moja mia tatu wakijeruhiwa kufuatia kutokea kwa tetemeko hilo baya.

Kupatikana kwa watu hao kumerejesha matumaini kwa waokoaji huenda wakaendelea kukuta watu waliohai zaidi baada ya hapo awali kuanza kukata tamaa ya kupata watu walio hai.

Serikali imeweka bayana kuwa tangu kuanza kwa zoezi la ukoaji sambamba na kusaka miili ya waliopoteza maisha imeshafanikiwa kuwapata watu mia moja na themanini na saba wakiwa hai na kuwanasua kutoka kwenye mabaki ya majengo.

Waziri wa Kilimo wa Uturuki Mehdi Eker amesema serikali yake itasambaza mifugo kwa wanavijiji ambao wamepoteza wanyama waokwa ajili ya kulipa fidia ya hasara ambazo wamezipata.

Uamuzi wa serikali umekuja baada ya jumla ya mifugo elfu tatu na themanini kupotea baada ya Uturuki kupigwa na tetemeko la ardhi lililotokea siku ya jumapili na kusababisha hasara kwa wananchi.

Serikali ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan imeendelea kuomba misaada na kukira kwamba imeshindwa peke yake kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi ambalo limeshuhudiwa katika nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.