Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UGIRIKI-UINGEREZA-UJERUMANI-UFARANSA

Viongozi wa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya EU kukutana nchini Ubelgiji kujadili mgogoro wa madeni

Viongozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya EU wanatarajiwa kukutana kwa mara nyingine katika Mkutano wa dharura ulioitishwa kwa ajili ya kushughulikia tatizo la madeni ambalo linaukumba Ukanda wa Ulaya ambao unatarajiwa kufanyika katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

REUTERS/Thierry Roge
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuria na vinara wa Umoja wa Ulaya EU akiwemo Rais wa Ufaransa Nicolas Srakozy, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

Mkutano huu unakuja baada ya viongozi hao kukutana siku ya jumapili huko Brussels lakini wakashindwa kufikia muafaka wa namna ya kuweza kushughulikia tatizo la madeni huku Uingereza ikikosolewa kutokana na kukataa kutumia sarafu ya euro kama nchi nyingine za Ulaya.

Viongozi hawa wanakutana kwa mara nyingine huko Brussels kutokana na kukumbwa na hofu huenda kile ambacho kinashuhudiwa nchini Ugiriki huenda kikasambaa katika nchi za Italia na hata Uhispani kutokana na nazo kuonekana uchumi wake kuanza kutetereka.

Nchi ya Italia imetakiwa kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya bajeti yake ili iweze kukabiliana na mtikisiko huo wa kiuchumi unaoshuhudiwa na tayari serikali ya Waziri Mkuu Silvio Berlusconi inaonekana inaweza ikakubaliana na mapendekezo hayo.

Viongozi kutoka nchi wanachama kumi na saba wanatarajiwa kukutana huku nchi za Ufaransa na Ujerumani ndizo zinaonekana kana vinara wa kushinikiza kuisadia nchi ya Ugiriki kuweza kujikwamua na madeni waliyonayo kwa kuipatia fedha zaidi.

Mkutano huu unatarajiwa huenda ukaibuka na majibu ambayo yanaweza yakasaidia kuondoa mgogoro wa madeni ambao yanaleta gumzo kwa uchumi wa Bara la Ulaya licha ya juhudi mbalimbali kufanyika kushughulikia suala hilo.

Mwaka huu pekee Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wameshakutana mara ishirini kushughulikia tatizo la kutetereka kwa uchumi lakini bado nchi za Ugiriki, Italia na Uhispania zimeendelea kukabiliwa na madeni makubwa huku uchumi ukipanda kwa kiwango kidogo mno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.