Pata taarifa kuu
UHOLANZI-TANZANIA-GAMBIA

Harakati za kusaka Mwendesha Mashtaka Mkuu Mpya wa Mahakama ya ICC zaiva

Mchakato wa kusaka mrithi atakayeziba nafasi ya Luis Moreno-Ocampo ambaye ni Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa ICC umezidi kuchanja mbuga wakati huu ambapo yametolewa majina manne ambayo yataamua nani achukua fursa hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa majima ambayo yanapatika kwenye orodha hiyo ya mwisho ni pamoja na waafrika wawili ambao ni Mwendesha Mashtaka Msaidizi wa ICC wa saa Fatou Bensouda na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman.

Majina mengine mawili ya wale ambao wanasaka nafasi ya Moreno-Ocampo kwa udi na uvumba ni pamoja na Mwendesha Mashtaka kutoka Mahakama Maalum wa Masuala ya Cambodia Andrew Cayley na Robert Petit ambaye anatoka Kitengo cha Sheria cha Canada.

Upatu umekuwa ukipigwa zaidi kwa wagombea hao kutoka Afrika kuweza kuchukua jukumu la kuendesha Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ICC baada ya muda mrefu nafasi ya Mwendesha Mashtaka kushikwa na watu kutoka mataifa mengine.

Hatua ya kupendekeza nafasi ya Mwendesha Mashtaka iende kwa mwafrika imekuja kutoka na kuonekana Mahakama ya ICC kuwashughulikia zaidi viongozi kutoka bara hili tofauti na ilivyo kwa wengine.

Bensouda ambaye ni raia wa Gambia awali kabla ya kuwa Mwendesha Mashtaka Msaidizi wa ICC alikuwa Mshauri Mwandamizi wa Sheria katika Mahakama Ya Mauji ya Kimbari ya Rwanda ICTR iliyopo Arusha, Tanzania.

Jaji Mkuu wa Tanzania Othman yeye anatajwa kama Mtaalam ambaye amebobea kwenye Sheria za Haki za Binadamu na amekuwa akifanya vyema kila sehemu ambayo ameshawahi kuhudumu.

Mwendesha Mashtaka ambaye atachaguliwa atakabiliwa na kibarua cha kuwasaka Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir pamoja na watu wa karibu wa Marehemu Kanali Muammar Gaddafi ambao wametolewa waranti ya kukamatwa.

Uchaguzi huo wa kusaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ICC unatarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa UN mwezi Desemba na mshindi ataanza majukumu yake mwezi Juni mwakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.