Pata taarifa kuu
UTURUKI

Matumaini ya kupata watu waliohai nchini Uturuki baada ya kupigwa na tetemeko yatoweka

Matumaini ya kuwapata watu waliohai nchini Uturuki baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi Mashariki mwa Taifa hilo siku ya jumapili na kusababisha vifo vya watu mia mbili na sabini na tisa na kuwajeruhi wengine zaidi ya elfu moja mia tatu yameanza kutoweka wakati huu Kikosi cha Ukoaji kikiendelea kusaka miili ya waliopoteza maisha.

REUTERS/Stringer/Turkey
Matangazo ya kibiashara

Matumaini hayo yametoweka baada ya Kikosi cha Ukoaji kuendelea kukutana na maiti za wale ambao wamenaswa kwenye vifusi lakini hadi sasa hakuna mtu aliye hai ambaye amepatikana kwenye msako ambao unaendelea kushika kasi ukiongoza na kikosi maalum.

Kikosi cha Ukoaji ambacho kinawajibu wa kusaka miili ya wale wote ambao wamenasa chini ya vifusi kimeonekana kikiendelea na juhudi zao wakati wananchi wakiendelea kushuhudia usiku wa pili wakiwa nje na kukabiliwa na baridi kali mno.

Serikali ya Uturuki imetangaza kuwa itatoa msaada wa haraka kwa wananchi ambao wameathirika na tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya matetemeko kwa saba nukta mbili.

Maofisa wa serikali wamesema kuwa jumla ya mahema elfu kumi na mbili yatatolewa katika Majiji ya Ercis na Van sambamba na vijiji vilivyojirani ambavyo navyo vimeshuhudia athari za tetemeko hilo baya kupiga nchi hiyo katika kipindi cha hivi karibuni.

Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki Bulent Arinc amethibitisha idadi ya vifo kufikia watu mia mbili na sabini na tisa huku watu wanaokadiriwa kufikia elfu moja na mia tatu wakijeruhiwa kwenye tetemeko hilo lililopiga nchi hiyo siku ya jumapili.

Tayari Waziri Mkuu Reccep Tayyip Erdogan alizuru eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi na kuwaahidi wananchi ya kwamba serikali kitakuwa bega kwa bega na wananchi ambao wamekumbwa na madhara ya tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.