Pata taarifa kuu
UTURUKI

Watu 217 wamepoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi nchini Uturuki

Zoezi la ukoaji na kusaka miili ya watu waliohai na bado wamefukiwa kwenye vifusi nchini Uturuki baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi Mashariki mwa taifa hilo lonaendelea kushika kasi hii leo Jumatatu wakati huu ambapo idadi ya waliokufa ikiongezeka na kufikia watu mia mbili na kumi na saba.

Matangazo ya kibiashara

Hofu imezidi kutanda huenda watu wengi zaidi wamefunikwa kwenye malundo ya vifusi baada ya eneo kubwa kuharibiwa na tetemeko hilo huku waokoaji wakishindwa kufika kwa haraka kutokana na miundombinu ya maeneo hayo kuharibika vibaya.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezuru eneo ambalo limekumbwa na tetemeko la ardhi katika Jimbo la Van kuangalia madhara ya tetemeko hilo lenye ukubwa wa saba nukta mbili huku akionya huenda idadi ya vifo ikazidi kwani bado watu wengi wamefukiwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Idris Naim Sahin amethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo akisema takwimu ambazo wanazo zinaonesha katika Jiji la Van wamefariki watu mia moja na Wilaya ya Ercis watu mia moja na kumi na saba wamepoteza maisha.

Meya wa Jiji la Van Bekir Kaya amesema majengo mengi yameharibiwa katika eneo lake huku mawasiliano yakikatika na kuchangia kwao kuzingirwa na ugumu wa kuweza kuwafikia wale ambao wameathiriwa na tetemeko hilo.

Kikosi maalum cha uokozi kikisaidia na wananchi wa kawaida wameendelea kuhakikisha wanawafikia watu walionaswa kwenye vifusi pamoja na miili ya wale ambao wamepoteza maisha na kufukiwa chini ya mabaki wa vifusi hivyo.

Takwimu zinaonesha kuwa watu zaidi ya elfu moja wamejeruhiwa hadi sasa kutokana na eneo la Mashariki mwa Uturuki kushuhudia likipigwa na tetemeko hilo baya la ardhi kuwahi kutokea katika kipindi cha hivi karibuni.

Uturuki imefanikiwa kuwakusanya wakoaji wapatao elfu moja mia mbili na sabini na tano wakiwa na magari ya kubebea wagonjwa mia moja na arobaini na tano kwa ajili ya kuharakisha kutoa huduma kwa waathirika.

Kumbukumbu zinaonesha mwaka elfu moja mia kenda na tisini na tisa Kaskazini Magharibi mwa Uturuki eneo lenye wingi wa viwanda na uchafuzi mkubwa wa mazingira kulishuhudiwa tetemeko baya la ardhi ambalo lilisababisha vifo vya watu elfu ishirini.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.