Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UBELGIJI

Serikali ya Ugiriki inasubiri kwa hamu huruma ya Umoja wa Ulaya EU kusaidia deni lake

Serikali ya Ugiriki inasubiri kwa hamu uokovu kwa uchumi wa nchi hiyo kutoka Umoja wa Ulaya EU baada ya Mawaziri wa Mambo ya Fedha kutoka wanachama wa Umoja huo kukutana huko Brussels nchini Ubelgiji na kukubaliana kuchangia €5.8 milioni kati ya €8 milioni zinazotakiwa na nchi hiyo.

REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

 

Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou ameelekea huko Brussels kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso kuangalia namna ya kuisaidia nchi hiyo baada ya Bunge kupitisha mapendekezo ya kubana matumizi yaliyopendekezwa na EU pamoja na Shirika la Fedha Duniani IMF.

Mkutano wa Mawaziri wa Fedha uliridhia kwa kauli moja kuweza kuisadia nchi ya Ugiriki ambayo inapita kwenye kipindi kigumu huku wananchi wa taifa hilo wakipinga vikali hatua ambazo zitataka kuchukuwa na serikali ili kuweza kuinusuru na janga linalowakabili.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki Evangelos Venizelos kwenye Mkutano huo amesema nchi yake si kitovu cha matatizo ya yanayotokea kwa sasa katika Ukanda wa Ulaya na badala yake usakwe ufumbuzi wa tatizo lililopo.

Mkutano huo unatarajiwa kuendelea hiyo kesho ambapo Viongozi wa Ulaya wakiongozwa na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel watauongoza kuangalia namna ya kuinusuru Ugiriki.

Waziri Mkuu wa Luxembourg wakati anawasili huko Brussels amenukuliwa akisema kunahitajika ufahamu mkubwa juu ya tatizo lililopo kwa sasa nchini Ugiriki na Barani Ulaya kwa ujumla ili kupata ufumbuzi.

Tatizo la mdeni katika Ukanda wa Ulaya lilianza nchini Ugiriki tangu hali kama hiyo iliposhuhidiwa katika nchi za Ireland na Ureno na sasa kuna tishio la kusambaa kwenye nchi za Italia, Uhispania na hata Ufaransa.

Mapema juma hili nchi ya Ugiriki imeshuhudia mgomo wa saa arobaini na nane ambao uliitishwa na Wafanyakazi wa umma ambao walikuwa wanapinga hatua mpya za kufunga mkanda za serikali ambazo hata hivyo zilipitishwa na Bunge nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.