Pata taarifa kuu
Malawi-ICC

Mahakama ya ICC yaitaka serikali ya Malawi ijieleze kwanini haikumkamata Omar Bashir

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC iliyoko mjini The Heague Uholanzi imeiandikia barua serikali ya Malawi ikiitaka nchi hiyo kutoa maelezo ni kwanini haikumkamata kiongozi wa Sudana Omary Hassan Al Bashiri anayetafutwa na mahakama hiyo.

Connectionivoirienne
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni rais Bashiri alihudhuria mkutano wa kikanda wa kibishara wa nchi wanachama wa ECOWAS huku nchi hiyo ikishindwa kumkamata kwa kile ilichodai sio wajibu wake kufanya hivyo na kiongozi huyo alialikwa kwenye mkutano huo.

Barua ya mahakama ya ICC inahoji ni kwanini serikali ya rais Bingu wa Mutahrika ilishindwa kumkamata rais Bashir wakati ikijua fika ilikwenda kinyume na sera za mahakama hiyo huku nchini yenyewe ikiwa ni mwanachama katika mahakama hiyo.

Mahakama ya ICC ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa rais Bashir kwa tuhuma za mauajo ya halaiki katika jimbo la Darfur hatua ambayo imepingwa vikali na umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.