Pata taarifa kuu
MONROVIA-LIBERIA

Upinzani nchini Liberia watangaza kupinga matokeo yote ya urais

Viongozi wa vyama viwili vya upinzani nchini Liberia wamekataa kuyatambua matokeo ya awali ya urais yaliyoanza kutangazwa na tume ya tiafa ya uchaguzi nchini humo kwa kile wanachodai kuwa tume hiyo inafanya njama kutaka kumpa ushindi rais wa sasa Bi Ellen Johnson Sirleaf. 

Mkuu wa Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Liberia James Fromayah akizungumza na waandishi wa habari mjini Monrovia
Mkuu wa Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Liberia James Fromayah akizungumza na waandishi wa habari mjini Monrovia REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na upinzani nchini humo imesema kuwa wanashangazwa na mwenendo wa utangazwaji wa matokeo ya urais nchini humo ambayo wamesema ni wazi yanampendelea mgombe wa chama tawala na kwamba hawatakuwa tayari kuyakubali hata matokeo rasmi yatakapotangazwa.

Hata hivyo tuhuma hizi zimekanushwa vikali na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo James Fromayah ambaye amesema madai hayo ya upinzani hayana ukweli wowote na kwamba matokeo wanayoyatangaza ni kwa mujibu wa kura ambazo zimehesabiwa mpaka sasa.

Matokeo ya awali yanaonyesha bi Sirleaf akiongoza kwa asilimia 44 ya kura wakati mpinzani wake Wiston Tubman akiwa na asilimia 36 ya kura ambapo ni majimbo kadhaa yamesalia kabla ya kutangazwa matokeo rasmi huku kukiwa na dalili ya kushuhudia duru la pili la uchaguzi nchini Liberia.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ina siku hadi ya tarehe 26 ya mwezi huu kutangaza matokeo rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.