Pata taarifa kuu
YEMEN

Maandamano mapya yazuka nchini Yemen

Maelfu ya wananchi wa Yemen wameandamana hii leo katika viunga vya mji mkuu Sanaa kwa siku ya pili mfululizo wakiendelea kushinikiza baraza la usalama la umoja wa mataifa UN kuchukua hatua dhidi ya utawala wa rais Ali abdulah Saleh.

Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa wameongezewa nguvu na mshindi wa tuzo la Nobel nchini humo mwanaharakati Tawakkul Karman's, waandamanaji hao wamelitaka baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuingilia kati machafuko yanayoendelea nchini humo.

Mjumbe wa baraza la umoja wa mataifa kwa Yemen Jamal Benomar amesema kuwa amepokea maombi ya wanaharakati na waandamanaji hao na kwamba anatarajiwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye kikao cha baraza hilo.

Rais saleh mwenyewe ameendelea kusisitiza kutong'atuka madarakani kwa shinikizo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.