Pata taarifa kuu
Umoja wa Ulaya

Viongozi wa Ulaya na harakati za kupambana na mdororo wa uchumi

Viongozi wa Mataifa ya Ulaya wakishirikiana na Benki ya Dunia, Benki ya Ulaya na Shirika la Fedha Duniani wanaendelea kuhaha kuhakikisha wanafanikiwa kukabiliana na hali mbaya ya kiuchumi ambayo inatishia bara hilo na dunia kwa ujumla.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ndiye aliyeongoza kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa jitihada za kuhakikisha wanadhibiti hali inayoshuhudiwa kwa sasa huku Rais wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso akisema wanampango mahsusi kukabili hali hiyo.

Wakati hali ikiwa hivyo Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza Mervyn King amenukuliwa akisema nchi yake imeamua kuongeza pauni bilioni sabini na tano kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi.

Naye Waziri wa Fedha wa Marekani Timothy Geithner hakusita kueleza namna ambavyo nchi yake inashiriki katika kupata suluhu ya tatizo la kuanguka kwa masoko kunakoshuhudiwa kila kukicha.

Suala hili linaonekana kugonga vichwa vya wengi kutokana na nchi ya Ugiriki kupitia kipindi kigumu kiuchumi hali ambayo imekuwa ikipokelewa kwa maandamano kutoka wananchi wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.