Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Mawaziri wa Fedha wa Ulaya kukutana kujadili mkopo wa Ugiriki

Mawaziri wa Fedha kutoka Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU wanatarajia kufikia maridhiano ya kuondoa vikwazo kwa kuipatia mkopo zaidi nchi ya Ugiriki ambayo inahaha kujinasua na hali ngumu ya kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Nchi wanachama kumi na saba kutoka Umoja wa Ulaya EU ambazo zinatumia sarafu ya euro zinakutana nchini Luxembourg kuangalia ushahidi wa kutosha wa kuikopesha au la Ugiriki jumla ya euro bilioni nane.

Mkutano huu unakuja baada ya miwshoni mwa juma kushuhudia Wakaguzi wa Mahesabu wa Kimataifa kuangalia namna ambavyo nchi ya Ugiriki inavyopambana kukabiliana na tatizo la kifedha ambalo linaikabili nchi hiyo.

Kamishna wa Uchumi na Masuala ya Fedha kutoka EU Olli Rehn anatarajiwa kutoa mchanganuo wa namna nchi ya Ugiriki ilivyo kiuchumi mbele ya Mawaziri wa Fedha kutoka Umoja huo.

Mkutano huu unakuja kutokana na hofu ambayo imeshaanza kutanda duniani ambayo inatilia shaka huenda uchumi wa dunia ukatetereka kutokana na hali halisi ilivyo nchini Ugiriki ikiendelea kuachwa.

Serikali ya Ugiriki yenyewe imeweka bayana inakabiliwa na hali ngumu zaidi kwani hata patoi lao la taifa limeendelea kuanguka katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011 ikitoka asilimia 10.5 hadi kufika asilimia 8.5.

Ugiriki imeweka bayana tumaini lake lililosalia katika kujiokoa kwenye janga hili la kuanguka kwa uchumi wao ni kwa Shirika la Fedha Duniani IMF na Umoja wa Ulaya EU ambao ndiyo wanaweza kuwa suluhu.

Ufaransa na Ujerumani ndiyo nchi ambazo zimeshaonesha utayari wake wa kutoa msaada ukiwemo wa mkopo kwa Ugiriki ili iweze kuepukana na hali ambayo wanapitia kwa sasa na kuiepusha dunia na janga.

Benki Kuu ya Ulaya ndiyo ambayo inatazamiwa kama mkombozi katika kuinusuru Ugiriki kuweza kukabiliana na hali mbaya ya kicuhumi ambayo inakabili taifa hilo kwa sasa.

Licha ya nchi hizo mbili kuonesha utayari wake wa kutoa msaada kwa Ugiriki lakini nchi nyingine zimekuwa zikitofautiana kwenye msamamo iwapo watoe mkopo kwa taifa hilo au waliache libane matumizi.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya sintofahamu wananchi wameendelea kutoa shinikizo kwa serikali wakiitaka iachane na sera yake ya kubana matumizi ambayo wamekuwa wakiona kama mbadala wa kukabiliana na tatizo hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.