Pata taarifa kuu
Yemeni

Rais wa Yemen arejea nchini mwake

Wakati harakati za kupinga uongozi wa Rais Ali Abdallah Saleh ambao umedumu kwa muda wa miezi saba sasa, hali ya uhasama imezidi kupamba moto katika siku za hivi karibuni. Mapigano kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais Ali Abdallah Saleh yameanza tena na hata kushika kasi. Ni katika hali hiyo Rais wa Yemen,ambae alikuwa anapatiwa matibabu nchini Saudi Arabia kwa miezi mitatu baada ya kutokea shambulizi nyumbani kwake, ameamua kurudi katika mji mkuu wa Yemen. Kurudi kwake kumewashtuwa wengi kwani haikutarajiwa kurejea kwake hivi karibuni.

Rais wa Yemeni Ali Abdallah Saleh arejea  Sanaa,septemba 23. 2011.
Rais wa Yemeni Ali Abdallah Saleh arejea Sanaa,septemba 23. 2011. REUTERS/Khaled Abdullah/Files
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Yemen hakutarajiwa kurejea nchini kwake katika siku za hivi karibuni, kwani katika kauli yake ya siku za nyuma alitangaza kumpa uwezo makamu wake kuendeleza majadiliano na upinzani, ishara kwamba hatorudi sasa hivi nyumbani kwake.

Katika siku tano zilizopita, mapambano makli yameshuhudiwa katika mji wa Sanaa, ambapo sasa kurejea ghafla kwa rais huyo inaonekana kuwa suluhisho pekee ya kurejesha utulivu katika nchi hiyo.

Hali ya usalama imekuwa ikizorota siku kwa siku katika mji mkuu. Mbali na mapambano ya kijeshi katika katikakati mwa jiji, mapigano mapya yameanzishwa katika maeneo mbalimbali. Jana risasi zilisikika kwenye chuo kikuu cha wanaombpinga Ali Abdallah Saleh. Wakati, kaskazini ya mji wa Sanaa wafuasi wa vyma mbalimbali vya kisiasa walishambuliana kwa risase.

Majadiliano baina ya upinzani na serikali yanayo simamiwa na wajumbe wa Umoja wa Mataifa pamoja na Baraza la Ushirikiano wa Ghuba hayajafikiwa makubaliano na yaonekana kuzoroto kufuatia mapendekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na kukataliwa na Rais Saleh.

Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.