Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu waahirisha ziara yao nchini Syria dakika za mwisho

Viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu waliokuwa wafanye ziara nchini Syria wameahirisha ziara hiyo kufuatia maombi ya kufanya hivyo toka kwa Serikali ya Syria iliyosema kwasababu za kiusalama.

Rais wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Nabil al Arabi
Rais wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Nabil al Arabi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kituo cha Televisheni cha Serikali, nchi hiyo ilimuomba mwenyekiti wa Umoja huo Nabil al-Arabi kuahirisha ziara hiyo kwa kile nchi hiyo ilichoeleza ni sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake.

Viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu walitarajiwa kufanya ziara nchini humo kuanzia hii leo ambapo walikuwa na lengo moja la kufikisha ujumbe wa kuundwa kwa Serikali ya vyama vingi kama ilivyokubaliwa na nchi wanachama.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa hatua ya Serikali ya Syria kuomba kuahirishwa kwa ziara hiyo kunatokana na kile kilichoelezwa ni msimamo wa Umoja huo kuhusu kutaka mabadiliko katika serikali ya rais Bashar al-Asad.

Wakati viongozi hao wakiahirisha ziara yao, kumeripotiwa kuuawa kwa watu wawili katika mji wa Homs siku ya Jumanne baada ya Polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji waliojitokeza kupinga utawala wa rais Asad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.