Pata taarifa kuu
UTURUKI-ISRAEL-MAREKANI

Umoja wa Mataifa UN kutoa ripoti ya mashambulizi ya Israel dhidi ya meli ya misaada ya Uturuki

Umoja wa Mataifa UN umeituhumu Israel kwa kutumia nguvu kubwa katika mpango wao wa kuzuia misaada isipelekwe kwenye Eneo la Ukanda wa Gaza mwaka 2010 ambapo Makomandoo wa nchi hiyo walivamia meli ya misaada ya Uturuki na kuua wanaharakati tisa.

Reuters/Emrah Dalkaya
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa UN kwenye ripoti yao ambayo imevuja na kuchapishwa kwenye Gazeti la New York Times imeeleza kuwa licha ya kutumika kwa nguvu kubwa lakini Israel ilikuwa na uhalali wa kuzuia meli hiyo kwa sababu za kiusalama.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa UN imebaini kuwa Israel ilipanga zoezi hilo la kuzuia meli za misaada zisipelekwe Eneo la Ukanda wa Gaza na kisha wakatumia nguvu kubwa kufanikisha hatua hiyo bila ya kujali haki za binadamu.

Meli ambayo ilishambuli ikiwa na bendera ya Uturuki ilikuwa imebeba shehena ya misaada ikiwa ni hatua ya kutaka kuwasaidia wananchi wa eneo la Ukanda wa Gaza ambao walikuwa wanahitaji misaada ya kibinadamu haraka.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa meli hiyo iliyobeba misaada kupelekwa eneo la Ukanda wa Gaza lilisababisha kuharibuka kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili ya Israel na Uturuki.

Ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kutolewa rasmi siku ya Ijumaa imevuja na kuweza kuandikwa kwenye gazeti na New York Times na kueleza namna ambavyo meli ya Mavi Marmara na nyingine vilivyoshambuliwa na makomandoo wa Israel.

Jopo la kuchunguza tukio hilo lilikuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa New Zealand Geoffrey Palmer ambaye ameweka bayana kisheria ilikuwa halali kwa Israel kuzuia meli hiyo kwani walikuwa wanajilinda na uingizwaji wa silaha.

Israel ilipotakiwa kuomba radhi baada ya kutokea kwa shambulizi hilo ilikataa na kusema wametekeleza kwa kufuata sheria za kimataifa hatua ambayo ilipingwa vikali na Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.