Pata taarifa kuu
Libya-Ufaransa

Ufaransa yataka ufanyike mkutano wa haraka kuhusu Libya

Ufaransa inataka ufanyike mkutano wa dharura wa nchi zinazo unga mkono waasi nchini libya ili kundaa mustakabili mzima wa nchi hiyo baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais kanali Muamar Gaddafi, hayo yametangazwa na waziri wa mambo ya nnje wa Ufaransa Alain Juppe.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe katika mazungumzo yake mafupi kwenye ikulu ya ufaransa Quai d'Orsay, huu ndio mwisho wa utawala wa Gaddafi uliodumu miaka 42.

waziri huyo amesema kwamba rais Nicols Sarkozy amewasiliana na mkuu wa waasi Moustafa Abdeldjeil, ambae atawasili nchini Ufaransa siku za usoni.

Waziri huyo amebaini kuwa kile walichokuwa wanateta kilikuwa kweli na kukumbusha kwamba Ufaransa na Uingereza zimekuwa katika safa ya kwanza katika kuwaunga mkono waasi katika muungano wa kimataifa ulioanza tangu Machi 19 baada ya azimio kupasishwa na baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa.

Alain Juppe amesema hatma ya Libya ipo mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe, jamii ya kimataifa itawasaidia kuhakikisha wanafaanikisha malengo yao.

Ufaransa inataka jamii ya kimataifa iliangalie swala kukutana haraka iwezekanavyo na kuwasaidia viongozi wapya wa libya, na ndio mana amesema waziri Juppe Ufaransa inataka ufanyike mkutano wa dharura wiki ijayo kujadili swala hilo.

Umoja wa Afrika, Umoja wa nchi za Kiarabu, UN, Umoja wa Ulaya na Marekani wanakaribishwa iwapo watapenda kushiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.