Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Syria wakati Rais Obama akimtaka Assad kuondoka madarakani

Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo vipya dhidi ya Utawala wa Syria chini ya Rais Bashar Al Assad na kusema hatua hiyo inalenga kudhoofisha nguvu za nchi hiyo kuendelea kushambulia waandamanaji.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hizi vinakuja wakati ambapo Rais wa Marekani Barack Obama ameshatangaza hatua ya kumtaka Rais Assad kuondoka madarakani hatua iliyoungwa mkono na washirika wake Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ametangaza vikwazo hivyo vinavyolenga biashara ya mafuta nchini Syria na kuzuia makampuni kutoka nchi humo kununua mafuta na hata bidhaa zake.

Vikwazo hivyo vinakwenda sambamba na kuzuiliwa kwa mali na fedha za serikali ya Syria ambavyo vipo nchini Marekani ili kuendelea kuipa wakati mgumu serikali ya nchi hiyo.

Waziri Clinton amesema hatua hii inakuja kudhihirisha maneno ambayo wamekuwa wanayaongea inabidi yaambatane na vitendo ili kudhibiti mauaji ambayo yanafanyika nchini Syria.

Clinton amesema mara kadhaa wamemtaka Rais Assad kuongoza kipindi cha mpito kwa lengo la kurejesha demokrasia nchini Syria lakini ameendelea kukaidi mapendekezo hayo na majeshi yake kufanya operesheni zaidi.

01:03

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akitangaza vikwazo dhidi ya Syria

Hivi ni vikwazo vipya ambavyo vimekuwa vikitangazwa na Marekani dhidi ya serikali ya Syria ambapo sasa mashirika yote hayatotakiwa kuthubutu kujihusisha na biashara za mafuta na nchi ya Syria.

Waziri Clinton ameahidi wataendelea na shinikizo zaidi kumtaka Rais Assad aondoke madarakani na tayari juhudi zao zimeaza kuzaa matunda baada ya nchi kadhaa kuwaunga mkono.

Tangazo la vikwazo limekuja baada ya mapema hii leo afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani kusema Rais Barack Obama amemtaka Rais Assad kuondoka madarakani kwa ajili ya mafanikio ya wananchi wa Syria.

Kauli ya kumtaka Rais Assad kuondoka madarakani imepata uungwaji mkono kutoka kwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

Mapema hii leo Msemaji wa Umoja wa Mataifa UN Farhan Haq alinukuliwa akisema Rais Assad amezungumza kwa njia ya simu wa Katibu Mkuu Ban Ki Moon na kumuahidi kusitisha operesheni ya kijeshi inayoendelea.

Tangu kuanza kwa kwa maandamano ya wananchi kushinikiza mabadiliko ya utawala nchini Syria zaidi ya watu elfu moja na mia nane wameuawa huku wengine zaidi ya elfu kumi wakiwa wanashikiliwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.