Pata taarifa kuu
LEBANON

Mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa yatoa ripoti ya uchunguzi kuhusu mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon

Mahakama maalumu iliyoundwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2007 (STL) kushughulikia kesi ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq al-Hariri imetoa ripoti inayoonyesha kuhusika kwa viongozi wanne wa Hezbollah na mauaji ya kiongozi huyo.

Waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq al-Hariri
Waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq al-Hariri Reuters/ Jamal Saidi
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hiyo ambayo pia imechapishwa kwenye tovuti ya mahakama ya umoja wa mataifa inayoshughulikia kesi hiyo imeweka wazi makosa matano ambayo yanawakabili watuhumiwa wanne wa chama kinachotawala hivi sasa nchini humo Cha hezbollah kwa kuhusika kwao katika mpango wa mauaji ya waziri mkuu rafiq al-Hariri.

Viongozi waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na Mustafa Amine Badreddine, Salim Jamil Ayyash, Hussein Hassan Oneissi and Assad Hassan Sabra ambao kwenye ripoti hiyo wameelezewa jinsi walivyoshiriki katika kuandaa mpango wa kutekeleza shambulio la kumuua kiongozi huyo.

Miongoni mwa makosa ambayo wanashtakiwa nayo viongozi hao ni pamoja na kushiriki vitendo vya kigaidi na kuandaa njama za kutaka kuipindua serikali iliyokuwa ikiongozwa na waziri mkuu Rafiq al-Hariri.

Mwezi wa sita mwaka huu mahakama hiyo ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa viongozi hao na kufikishwa mbele ya majaji kujibu tuhuma za mauaji zinazowakabili huku tayari kundi la Hezbollah kupitia kwa msemaji wake limekataa kushirikiana na mahakama hiyo.

Hata hibyo wachambuzi wa masuala ya sheria za kimataifa wamekosoa ripoti hiyo wakidai kuwa ina mapungufu kwa kuwa imeshindwa kuwahusisha maofisa wa usalama wa nchi ya Israel ambao wanatajwa pia kuhusika katika kusuka mpango wa mauaji ya Rafiq Hariri.

Waziri mkuu wa Rafiq al-Hariri aliuawa mwezi wa pili mwaka 2005 ambapo baada ya kifo chake mtoto wake Saad Hariri alichukua madaraka kabla ya kushuhudia pia hata yeye mwenyewe akilazimika kuondoka madarakani kwa shinikizo la chama cha Hezbollah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.