Pata taarifa kuu
Yemen

Kurejea kwa rais wa Yemen nchini mwake siku za usoni

Serikali nchini Yemen imetangaza kuwa hivi karibuni rais wa taifa hilo Ali Abdullah Saleh atarejea nchini humo akitokea Saudi Arabia alikokuwa akipatiwa matibabu maofisa wa serikali wamedhibitisha.

Contrepoints
Matangazo ya kibiashara

Maofisa hao wamedai kuwa rais Saleh atarejea nchini mwake baada ya madaktari wanaomtibu kutoa taarifa rasmi kuhusiana na maendeleo ya afya yake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya shambulio la roketi katika ikulu yake miezi michache iliyopita.

Wakati rais Saleh akitangaza kuwa atarajea nchini nyumbani hivi karibuni ikulu ya Marekani imemtaka rais Saleh kutorejea nchini mwake na kuruhusu kufanyika kwa mabadiliko ya serikali ili kuepusha machafuko zaidi nchini humo.

Mara ya mwisho rais Salehalionekana kwenye televisheni tareh 7 mwezi wa 7 akiwa na bandeji kichwani na kutoa tuhuma kwa mataifa ya ulaya kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyotaka kupindua serikali yake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.