Pata taarifa kuu
Norway

Anders Behring Breivik kusikilizwa kesho na polisi

Polisi nchini Norway wanasema kuwa, kesho Ijumaa watamhoji Anders Behring Breivik mwanaume mwenye umri wa miaka 32 aliyekiri kuwauawa watu 76 juma lililopita kwa kuwapiga risasi na kutekeleza shambulizi la bomu jijini Oslo.

Anders Behring Breivik
Anders Behring Breivik REUTERS/Jon-Are Berg-Jacobsen
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema kuwa wametamatisha uchunguzi wa kuwasaka watu wengine wanaosemekana kupotea katika kisiwa cha Utoeya, eneo la mkasa huo.

 
Waziri Mkuu wa Norway,Jens Stoltenberg anasema serikali yake haitatishwa na shambulizi hilo na anaamini kuwa uchunguzi utabaini mengi zaidi kuhusu mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.